Umri Mwafaka Zaidi Wa Kupata Mtoto Kwa Binti

Umri Mwafaka Zaidi Wa Kupata Mtoto Kwa Binti

A woman should get pregnant when she feels she is most ready to become a mother. However, age can play a factor in planning the pregnancy. Dr Ann Tan, Fertility Specialist from Mount Elizabeth Hospital tells you how to plan a healthy pregnancy in your 20s, 30s and 40s.

Je, ni umri upi ulio sawa kupata mtoto?

Ni umri upi unaofaa wa kupata mtoto? Huenda ukawa uko katika umri wako wa miaka 20, 30 ama 40 unapo amua kupata mimba. Huenda pia unajiuliza ni wakati upi bora wa kuweza kupata motto.

Uamuzi unalingana na mahali ulipoko maishani-vile ambavyo safari yako imekuwa na mahala unapoelekea. Je, ulipatana na mwenzio mapema maishani? Ungetaka familia kubwa? Walakini, umri sio nambari tu ikifika wakati wa kupata mimba. Iwapo kila mimba si sawa na nyingine, vitu mbali mbali vya kisia na kifisikia vinalingana na umri.

Umri mwingi huathiriwa na matatizo mengi ya kiafya kwako na kwa mwanao. Walakini, kama mama mchanga, huenda hauna uzoefu wa kutosha wa maisha wa jinsi ya kupambana na changamoto za ki hisia, fedha, na saikolojia yanayo ambatana na uja uzito na kujifungua.

Katika nakala hii, tunakusaidia kufahamu faida na hatari zinazo husiana na kuwa mja mzito katika umri wa miaka 20, 30 na 40.

Tuliongea na daktari Ann Tan, mtaalam wa uzazi kutoka Hospitali ya Mount Elizabeth iliyoko Singapore, ili kupata habari zaidi ya jinsi unavyo weza kuipanga mimba yako ya afya zaidi katika karne hizi.

Are your 20s the right age to have a baby? In your 20s you may just be settling into a new marriage and may not be ready for a baby.

Katika Miaka Yako ya 20’s, Huenda Ikawa Umeoleka Karibuni Na Huko Tayari Kupata Mtoto

Umri sawa kupata mtoto

Katika miaka yako ya 20, mwili wako utayari kupata mtoto lakini, je, wewe uko tayari?

Mwili wako uko mahali pema zaidi kupata mimba katika umri wa miaka 20. Mzunguko wa hedhi yako huwa sawa na mayai yako( kwani, ulizaliwa na kiasi kikubwa cha mayai) yako safi na yenye afya bora huku kufanya conception kuwa rahisi zaidi.

Kiwango cha juu cha mayai bora inapunguza hatari za matatizo ya kimaumbile.

Huu pia ni umri ambao mwili wako unaweza kupambana na fikira nyingi za uja uzito, mgongo na misuli. Ujana wako una maanisha kuwa ni vigumu kwako kupata matatizo ya uja uzito. Kwa hivyo kuongea kwa kifizikia, umri wako wa miaka 20 ndio wakati bora zaidi kwako kupata mtoto.

Walakini, mwili wako kuwa tayari kwa jambo hili halina maana kuwa wewe mwenyewe u-tayari. Kuna uwezekano umeanza career yako ama umeoleka hivi karibuni unapokuwa wa miaka 20. Huenda katika wakati huu, hauko tayari kwa mabadiliko haya yanayo sababishwa na kuwa mzazi na kugeuza maisha yako.

Kwa hivyo, miaka michache tu huenda ikawa na tofauti kubwa sana. Iwapo u-katika miaka yako ya mwisho ya 20, huenda ukahisi uko tayari kifedha na una uhusiano bora na kazi na uko tayari kufanya uamuzi wa kuwa mja mzito.

Umri sawa kupata mtoto: Miaka 30, miaka na mayai yako imekomaa

Katika umri huu, unahisi uko tiyari ki hisia, psykologia na kifedha kuanza familia kulinganishwa na unapokuwa katika umri wako wa 20s. Katika nchi kama Singapore, umri average wa mama wa mara ya kwanza ni miaka 30s.

Walakini, unapo endelea kukomaa, mayai yako pia yana komaa, na kufanya kutunga mayai kuwa jambo gumu. Unapo pata mimba katika miaka yako ya mapema ya 30s, utapata kuwa fikira nyingi za kifizikia hazina tofauti nyingi na unapokuwa katika umri wa miaka yako ya 20s. Idadi yako ya fitness na energy haina tofauti na mwanamke  aliye na mimba katika umri wake wa miaka ya mwisho ya 20s, haswaa unapozingatia maisha yenye afya bora.

Ila unapo fika miaka ya kati ya 30s, mambo yanabadilika.

Umri wa miaka 35 ni wakati ambapo uja uzito huwa rasmi “hatari ya juu”.  Unakuwa katika hatari ya matatizo ya uja uzito kama vile gestational diabetes, ila chances za mwanao kuzaliwa na matatizo ya chembeuzi kama vile Down Syndrome, huongezeka kila mwaka baada ya miaka 35.

Kukumbana na jambo hili, ni muhimu kumtembelea na kujadili na daktari wako vipimo ambavyo unapaswa kuchukua ili kuituliza akili yako. Vipimo vya uchunguzi ili kufanya uamuzi ni kama vile kipimo cha triple ama cha nuchal translucency.

Iwapo kipimo cha screening kinaonyesha hatari ya juu ya Down Syndrome, vipimo vya kidiagnosia vina weza kufanywa ili kubainisha iwapo mtoto ana Down Syndrome. Kama vile amniocentesis ambapo sampuli ya maji ya amniotic inayomzunguka mtoto inatolewa kutumia sindano iliyo ingizwa katika tumbo la mama. Ama sampuli ya Chorionic Villous (CVS)inayo husisha kuchukua sampuli ya celi kutoka kwenye kondo la nyuma la mama kupima jeni za mtoto.

Pia unahitaji kuongea na daktari wako kuhusu njia ya kuzingatia afya bora katika uja uzito.

Katika umri wako wa 40s, inakuwa vigumu zaidi

Kutoka ona ya kimatibabu, hii ndio karne ngumu zaidi na yenye hatari zaidi kujaribu kupata mtoto.

Kwa wakati huu, umebaki na mayai yenye ubora wa chini na kufanya kutunga mimba kuwa pole pole zaidi. Ila kwa uhakika, unaweza kumtembelea daktari wako kupata matibabu ya uzazi na upate msaada na jambo hili.

Katika miaka yako ya 40’s, kuna uwezekano yako kupoteza mimba , kupata matatizo ya ki afya ya uja uzito na mtoto wako kuzaliwa na matatizo ya chembeuzi huwa juu zaidi. La kufurahisha zaidi ni kuwa, umri wa juu zaidi ambao ni hatari kwako kupata mtoto pia huwa rahisi kwako kupata mapacha.  Hii inajulikana kama mimba ya hatari zaidi.

Utahitajika kumtembelea daktari wako mara kwa mara, kuhakikisha kuwa kondo lako la nyuma na mwanao wanakua vizuri na pia kwa hali yako ya mama mja mzito.

Kwa upande chanya, unapopita changamoto hizi zote, kuna uwezekano uko tayari kuwa mama. Huenda umejipanga kifedha, na umekamilisha maono mengi yako ya kibinafsi na ya kimasomo na kukuweka huru kuwa mama.

umri sawa kupata mtoto

Wanandoa Wote Wanao Kusudia Kupata Watoto Wanapaswa Kuenda Kufanyiwa Vipimo Vinavyo faa.

Mbali na umri wako, hakikisha umefanyiwa vipimo vya afya kabla ya kutunga mimba

Iwapo hamna umri sawa wa kupata mtoto, ni muhimu kwa kila wana ndoa kuhakikisha kuwa wana afya bora kabla ya kupanga uja uzito. Jambo hili litatoa shaka yoyote kuwa mayai ama shahawa ziko katika hali njema kabla ya kupata mimba.

Tembelea mtaalam wa uzazi ambaye atakushauri kupata kipimo cha kawaida ama kirefu kama inavyo hitajika. Chaguo la kipimo lita tegemea na historia ya familia ya wana ndoa na pia historia yao ya matibabu.

Vipimo vya kawaida vinavyo fanywa kabla ya kutunga mimba hupima iwapo wazazi hawa wana:

  • Matatizo yoyote ya kimatibabu au shida za jeni
  • Virusi vyovyote vya kingono
  • Magonjwa ya immunological
  • Kugundua ukosefu wa iron na vitamini D

Kwa kuongeza, kuna kipimo kingine ambacho kinaweza kuonyesha hali ya mayai ya mama. Kipimo hiki kina pima idadi ya homoni ya Anti Mullerian- idadi ya juu ya homoni hii huongeza idadi ya mayai na kuongeza nafasi yake ya kuwa na mimba.

Walakini, idadi ya juu zaidi huenda ikaonyesha hatari ya polycystic ovarian syndrome. Somo la AMH ni muhimu kwa wanandoa waliokomaa ama wanawake walio fanyiwa upasuaji wa ovaries kama vile kutolewa cyst.

Umri sawa kupata mtoto: Matatizo ya kiafya ambayo kila mwanamke anapaswa kufahamu kabla ya kuamua kupata mtoto katika umri wowote ule

Iwapo wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya 35 na haswa walio katika umri wao wa 40 wako kwa hatari ya kupata matatizo ya kiafya kufuatia shida za kiafya, kuna matatizo ambayo huenda yaka athiri wanawake wachanga na wazee pia. Kama vile:

  • Polycystic Ovarian Syndrome (PCOS), tatizo linalo wakumba wanawake wanao pata hedhi zisizo fuatana na ila pia wanapo, wakati mwingi hawapati ovulation.
  • Pelvic inflammatory disease, ambayo kwa mara nyingi husababisha uharibifu wa tubal ama kuzibika.
  • Pelvic endometriosis, inayo sababisha kuharibika kwa ovari na huenda ikapunguza ubora wa mayai yanayo tolewa, na pia kuziba harakati za shahawa kuelekea kwa ovari kufuatia kujitoa kwa pelvic.
  • Nyuzi za nyuzi(fibroids), ambazo zinaweza kuharibu uterine cavity.
  • Endometrial polyps, inayo zuia  uingiwaji(implantation).
umri sawa kupata mtoto

Wazazi Wa Kiume Pia Wanafaa kuwa Na Afya Njema Na Miaka Pia.

Umri sawa kupata mtoto: Weka akilini umri wa baba pia

Sio umri wa mama pekee ambao mmoja anapaswa kuangalia. Umri wa baba pia ni muhimu. Baba anapo zeeka, ubora wa shahawa yake hupungua, kupitia kuongezeka kwa umri na kupunguka kwa idadi ya testerone mwilini.

Iwapo mwanamme anaye elekea kuwa baba amekuwa akikunywa madawa kufuatia hali yake ya kiafya, huenda ika athiri ubora wa shahawa.

Ongezeko la umri wa baba lime husishwa na hatari iliyo ongezeka ya autism katika watoto wao.

Maisha bora huenda yakafanya uja uzito kuwa rahisi zaidi

Haijalishi umri unao amua kupata mtoto, kumbuka kula vizuri, kufanya zoezi mara kwa mara na upunguze fikira nyingi maishani mwako. Iwapo mwili wako na akili ziko katika afya bora, huenda ikafanya uja uzito wako kuwa rahisi zaidi kwako.

Pia kumbuka, mbali na umri ulio sawa kupata mtoto, jaribu kupata mtoto wakati ambapo wewe na mpenzi wako mko na afya njema, magonjwa yaweza kuwa na athari hasi kwa ubora wa mayai na manii.

Written by

Risper Nyakio