Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Vita Vya Kindoa: Kwa Nini Wanandoa Huwa Na Vita Mara Kwa Mara

3 min read
Vita Vya Kindoa: Kwa Nini Wanandoa Huwa Na Vita Mara Kwa MaraVita Vya Kindoa: Kwa Nini Wanandoa Huwa Na Vita Mara Kwa Mara

Vita vya kindoa huwa maarufu katika ndoa, ila vinapokuwa vya mara kwa mara, kuna tatizo katika ndoa yenu na mnapaswa kulisuluhisha.

Wanandoa ni watu wawili tofauti walio na maoni na utambuzi maishani kwa hivyo inatarajiwa kuwa mabishano na vita vitatukia. Lakini itakuwaje iwapo vita hivi vinatendeka mara kwa mara? Ina maana kuwa wanandoa hawapendani tena? Je, ndoa yao ina nafasi ya kufuzu? Nini chanzo cha vita vya kindoa?

Vita Vya Kindoa

vita vya kindoa

  1. Kukosa kuwasiliana

Wanandoa wengi hubishana kwa sababu hawaelewani na hii sio kwa sababu hawajuani vyema. Wanabishana kwa sababu hazungumzi kuhusu hisia zao kwa wachumba wao. Wanafanya uamuzi wa kunyamaza hadi mambo yanapolipuka. Jambo hili linaendelea kila mara wanandoa wanapobishana kuhusu chochote.

Wanandoa wanapaswa kujifunza kuzungumza kuhusu hisia zao bila kukasirika. Wanapaswa kuelewa kuwa wachumba wao hawana uwezo wa kusoma akili zao na hawajui jinsi watakavyo hisi wasipo waambia. Wanapo zungumza, wanapaswa kudumisha mawazo wazo na kiwango fulani. Kuzungumza mara kwa mara ni lazima kwa wanandoa ili kuepuka vita.

2. Ngono

Wanandoa huteta kuhusu ngono - kuwa hawapati ya kutosha ama ni nyingi sana. Baadhi ya wakati, ni kwa sababu mtu mmoja anajipenda na hajali kuhusu kumtosheleza mwenziye.

Haijalishi tatizo la kingono la wanandoa ni nini, wanapaswa kuwa na uraibu wa kufanya mapenzi. Ongezeko la mapenzi liliko wanandoa wanapo kumbatiana ama kubusiana kunaweza fungua nafasi nyingi kurekebisha kinacho watatiza katika idara ya mapenzi. Baada ya muda, wataweza kutatua suala hili.

3. Nani mkuu

vita vya kindoa

Watu wanaofikiria kuwa hawana doa wakati wote huingia kwa mabishano. Hii ni kwa sababu wanajikinga na kukataa kukubali kisicho sawa. Kiburi ni muhimu katika kudumisha kujithamini kwa mtu, lakini watu walio na kiburi kikubwa hawapendwi na wengine.

Mtu hapaswi kutii mchumba wake wakati wote. Lakini kusema pole na kukubali anapokosea ni hitaji mtu anapokuwa katika uhusiano kwani hupunguza kubishana kusikofaa.

4. Wapenzi wa hapo awali

Kuna watu wasioweza kuwachana na maisha yao ya hapo awali na kushindwa kuwachana na wachumba wao wa hapo awali. Mara nyingi, hujilinganisha na wachumba wao wa hapo awali. Sio vyema na kuna haribu viwango vya kujithamini kwa mtu.

Mambo ya hapo awali yanapaswa kubaki nyuma. Wanandoa wanapaswa kusahau kuhusu maisha yao ya hapo awali na kuwa makini na kinachofanyika. Haijalishi iwapo ana mwili unaovutia zaidi ama kazi inayolipa vyema zaidi. Zingatia kuwa mtu bora zaidi na uhusiano ulio nao kwa sasa.

5. Mazoea yanayo kukera

Watu wote wanatabia za kukera lakini kinacho anza vita vya kindoa ni kuwa hawataki angalau kubadilika na kuwachana na tabia hizi. Ni vigumu kuwacha tabia ulizo zoea lakini kumsumbua mchumba wako mara kwa mara itafanya iwe vigumu zaidi. Badala ya kumsumbua kila mara, mwulize kwa heshima kuhusu kitu kimoja ambacho hukipendelei na ambacho ungependa abadilishe. Kuelewana husaidia wakati wote.

Vita katika uhusiano hakumaanishi kuwa ndoa haitafanya kazi. Ni kujaribu kutopigana ambako hufanya ndoa zisifuzu. Unafikiria kwa nini wanandoa huwa na vita? Una sababu nyingine ambayo ungependa kutujulisha kuhusu?

Soma Pia: Wanandoa Wanapopigana Kuhusu Ngono Na Suluhu Lake

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Relationship & Sex
  • /
  • Vita Vya Kindoa: Kwa Nini Wanandoa Huwa Na Vita Mara Kwa Mara
Share:
  • Hofu 3 Maarufu za Ndoa Zinazowafanya Watu Kuogopa Ndoa

    Hofu 3 Maarufu za Ndoa Zinazowafanya Watu Kuogopa Ndoa

  • Ishara 5 Kuwa Hauko Tayari Kufunga Ndoa

    Ishara 5 Kuwa Hauko Tayari Kufunga Ndoa

  • Mambo 3 Ya Kufanya Unapomshuku Mchumba Wako Kuwa Na Mpango Wa Kando

    Mambo 3 Ya Kufanya Unapomshuku Mchumba Wako Kuwa Na Mpango Wa Kando

  • Hofu 3 Maarufu za Ndoa Zinazowafanya Watu Kuogopa Ndoa

    Hofu 3 Maarufu za Ndoa Zinazowafanya Watu Kuogopa Ndoa

  • Ishara 5 Kuwa Hauko Tayari Kufunga Ndoa

    Ishara 5 Kuwa Hauko Tayari Kufunga Ndoa

  • Mambo 3 Ya Kufanya Unapomshuku Mchumba Wako Kuwa Na Mpango Wa Kando

    Mambo 3 Ya Kufanya Unapomshuku Mchumba Wako Kuwa Na Mpango Wa Kando

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it